Showing posts with label adpollex. Show all posts
Showing posts with label adpollex. Show all posts

Sunday, April 7, 2019

Kampuni ya matangazo ya ADPOLLEX nchini yatoa offer mpya kwa wale wanaotaka kutangaza biashara zao kimataifa

adpollex
Kampuni ya matangazo ya ADPOLLEX iliyojikita Afrika Mashariki kwenye shughuli za utangazaji sasa imezindua offer mpya ya kukupa nafasi mteja wetu kutangaza biashara/kampuni yako kimataifa kwa sasa kampuni imeaonyesha nia ya dhati ya kuwekeza kwa wajasiriamali wadogowadogo hili kuwazesha wafanyabiashara wadogo kuwekeza kwenye matangazo ili kuongeza mapato yao. Uwekezaji huu unatarajiwa kuongeza tija na muamko wa wafanyakazi na wateja wao. Kufuatia mabadiliko haya sasa kampuni ya ADPOLLEX  itaweza kuhudumia wateja wake kwa viwango vya juu zaidi huku idadi ya wabunifu na vitendea kazi vikiongezwa.
Akizindua OFFER hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwekezaji huyo Bwana CHRISPER MALAMSHA amesema, “nia na madhumini ya uzinduzi huu ni kuitambulisha kampuni hii kwa upya kwa watanzania, licha ya kuwapo hapa nchini kwa zaidi ya miaka miwili.
MALAMSHA aliendelea kusema “soko la Tanzania kwa sasa linakua kwa kasi na sekta ya ushirikiano inazidi kukua kwa viwango vya juu, hivyo umuhimu wa kutangaza masoko na bidhaa zinazozalishwa ni mkubwa mno, kwa kufanya hivi tunatoa nafasi kwa makampuni mengine kutambua uwepo wetu hapa Tanzania na Afrika mashariki na wao kuweza kuzitambua kazi tunazozifanya.
”Kufuatia uwekezaji huu mpya na kukutangazia kampuni yako kimataifa, nia kubwa ni kukuza sekta ya masoko kwa Afrika mashariki huku tukifanya kazi kwenye viwango vya kimataifa. Tunayofuraha kubwa kwa uwekezaji huu kwani utaongeza tija kwa watanzania wenye vipaji.
Kampuni ya ADPOLLEX inatoa huduma mbalimbali kama kuandaa matangazo ya biashara kwa niaba ya wateja, kununua nafasi za matangazo kwenye vyombo vya habari, kuandaa mikakati ya jinsi ya kukuza bidhaa yako, kuwatangazia wateja bidhaa zao kwenye mitandao mbalimbali na kuwashauri hali halisi ya masoko na ushindani ilivyo duniani kwa sasa.
“Ni furaha kubwa kuitambulisha kwenu kampuni ya ADPOLLEX” alisema Bw Daniel Octavian, Meneja Mkuu wa ADPOLLEX Tanzania, huku tukijivunia timu yenye wafanyakazi bora na kazi nzuri ambazo tumeshazifanya mpaka sasa kwa wateja wetu,licha ya kuandaa kazi nzuri zilizoendana na soko la wateja wetu lakini pia tumeonekana kimataifa na kupata nafasi ya kushiriki kwenye baadhi ya forum mbalimbali duniani kwenye sekta ya matangazo. Ushiriki huu utakuwa na manufaa makubwa kwa wateja wetu na kutuwezesha sisi kama ADPOLLEX kupanua wigo wetu wa kufanya kazi kimataifa.
Dhamira yetu ni kuona ushindani wa matangazo ya bidhaa kwa Tanzania unakua na kufikia viwango vya kimataifa.
Bw Daniel aliendeela kusema “Kama kampuni tumefanya kazi hapa Tanzania kwa miaka miwili na makampuni ya ndani na nje ya Tanzania ikiwamo makampuni ya simu, benki, taasisi zisizo za kiserikali,kampuni za samani za ndani, kampuni za sola na nyingine nyingi. Kwa miaka hiyo michache ya kufanya kazi kwa bidii na kutambulika kimataifa,kampuni ya ADPOLLEX sasa inasababu ya kujivunia ujuzi wa kufanya kazi za wazawa huku tukizifanya kwa viwango vya kimataifa. Kama wadau wa matangazo tunaamini ubunifu bora unaleta ushindani katika soko na kuweza kuifikisha bidhaa kwenye viwango vya kimataifa.
GudyTV

Saturday, April 22, 2017

Njia Tano (5) Bora Za Kupata Mtaji Wa Kuanza Au Kukuza Biashara


Moja ya changamoto ambazo watu wengi wanaotutafuta huwa ni wanawezaje kupata mtaji wa kuanza biashara. Hiki kimekuwa kikwazo kwa watu wengi kuingia kwenye biashara. Hata wale ambao tayari wapo kwenye biashara, wamekuwa wakitamani kukuza biashara zao ila wanashindwa kutokana na kukosa fedha za kuingiza kwenye biashara.

Tatizo kubwa ambalo linawazuia wengi kutopata mtaji wa biashara ni kwa sababu inapokuja swala la mtaji wanafikiria sehemu moja tu, ambayo ni mkopo. Na kwa bahati mbaya sana watu wengi wanakuwa hawana sifa zinazowawezesha kupata mkopo wa kibiashara. Kwa kukosa sifa hizo huishia kukaa na kulalamika nataka kuingia kwenye biashara ila mtaji sina.

Kama wewe unapenda biashara, na umepanga kuingia au umeshaingia lakini hujaweza kukuza mtaji wako, hapa tutakupa njia mbalimbali za kupata mkopo kwa ajili ya biashara yako.


  1. Fedha zako binafsi.
Njia nzuri sana kwako kupata mtaji wa biashara ni kwa kuanza kuweka akiba ya fedha zako mwenyewe. Kama umeajiriwa anza utaratibu maalumu wa kuweka kiasi cha fedha pembeni ambacho hutakigusa hata iweje. Baadae unaweza kukitumia kwenye kuanza biashara. Kama hujaajiriwa unaweza kutafuta shughuli yoyote ukafanya na hii ikakuingizia kipato ambacho baadae utaweza kuanzia biashara.


  1. Michango kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki.
Kama unaweza kukaa chini na ndugu zako na ukawashawishi vizuri, watakuwa tayari kukuchangia uanze biashara. Kama watu wanaweza kuchangia harusi na mambo mengine, wanaweza pia kuchangia biashara, ni wewe uweze kuwashawishi vizuri. Ila hapa unahitaji kuwa unaaminika na ndugu hao n apia waoneshe ni jinsi gani wao watanufaika na biashara utakayoanzisha.


  1. Kutafuta mtu au watu wa kushirikiana nao.
Kwa uzoefu wetu, kuna watu wengi ambao wana mitaji ya kibiashara ila hawajui ni biashara gani wafanye au hawana muda wa kusimamia biashara. Na wakianzisha biashara kwa sababu hawana usimamizi mzuri wanapata hasara. Sasa wewe unahitaji kuwajua watu wa aina hii na andaa mpango ambao utawashirikisha na kuonesha ni kwa jinsi gani mkiungana pamoja mnaweza kuwa na biashara nzuri na yenye faida. Hii pia inahitaji uwe unaaminika na yule unayempelekea mpango wako.


  1. Kuanza biashara kwa fedha za mteja.
Hapa unaweza kukusanya fedha kwa wateja kwanza halafu ndio ukawapata huduma au bidhaa wanayohitaji. Kama utaweza kuwa na mpango mzuri wa biashara ambapo mteja anahitaji sana unachotoa, na tayari anakuamini anaweza kukupa sehemu ya gharama na wewe kutumia gharama hiyo kumpatia bidhaa au huduma anayotaka. Hii pia inahitaji uaminifu na wale unaofanya nao biashara.

Hii ndio njia ambayo inafahamika na kila mtu na watu ndio huwa wanaifikiria hii kila wanapofikiria mkopo wa biashara. Kama una sifa za kupata mkopo unaweza kuchukua mkopo na kuutumia kwenye biashara. Ila kuwa makini sana kama unachukua mkopo kwa ajili ya kuanzia biashara, ni hatari sana na unaweza kujiingiza kwenye matatizo zaidi.

Bado unafikiria ni njia gani unazoweza kutumia kupata mkopo wa biashara? Anza na hizo hapo juu na boresha kadiri biashara yako ilivyo na wale wanaokuzunguka walivyo. Hakuna kitu kinachoshindikana kama utaamua kweli kupata mkopo wa biashara.