Showing posts with label Masoko. Show all posts
Showing posts with label Masoko. Show all posts

Sunday, April 7, 2019

Kampuni ya matangazo ya ADPOLLEX nchini yatoa offer mpya kwa wale wanaotaka kutangaza biashara zao kimataifa

adpollex
Kampuni ya matangazo ya ADPOLLEX iliyojikita Afrika Mashariki kwenye shughuli za utangazaji sasa imezindua offer mpya ya kukupa nafasi mteja wetu kutangaza biashara/kampuni yako kimataifa kwa sasa kampuni imeaonyesha nia ya dhati ya kuwekeza kwa wajasiriamali wadogowadogo hili kuwazesha wafanyabiashara wadogo kuwekeza kwenye matangazo ili kuongeza mapato yao. Uwekezaji huu unatarajiwa kuongeza tija na muamko wa wafanyakazi na wateja wao. Kufuatia mabadiliko haya sasa kampuni ya ADPOLLEX  itaweza kuhudumia wateja wake kwa viwango vya juu zaidi huku idadi ya wabunifu na vitendea kazi vikiongezwa.
Akizindua OFFER hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwekezaji huyo Bwana CHRISPER MALAMSHA amesema, “nia na madhumini ya uzinduzi huu ni kuitambulisha kampuni hii kwa upya kwa watanzania, licha ya kuwapo hapa nchini kwa zaidi ya miaka miwili.
MALAMSHA aliendelea kusema “soko la Tanzania kwa sasa linakua kwa kasi na sekta ya ushirikiano inazidi kukua kwa viwango vya juu, hivyo umuhimu wa kutangaza masoko na bidhaa zinazozalishwa ni mkubwa mno, kwa kufanya hivi tunatoa nafasi kwa makampuni mengine kutambua uwepo wetu hapa Tanzania na Afrika mashariki na wao kuweza kuzitambua kazi tunazozifanya.
”Kufuatia uwekezaji huu mpya na kukutangazia kampuni yako kimataifa, nia kubwa ni kukuza sekta ya masoko kwa Afrika mashariki huku tukifanya kazi kwenye viwango vya kimataifa. Tunayofuraha kubwa kwa uwekezaji huu kwani utaongeza tija kwa watanzania wenye vipaji.
Kampuni ya ADPOLLEX inatoa huduma mbalimbali kama kuandaa matangazo ya biashara kwa niaba ya wateja, kununua nafasi za matangazo kwenye vyombo vya habari, kuandaa mikakati ya jinsi ya kukuza bidhaa yako, kuwatangazia wateja bidhaa zao kwenye mitandao mbalimbali na kuwashauri hali halisi ya masoko na ushindani ilivyo duniani kwa sasa.
“Ni furaha kubwa kuitambulisha kwenu kampuni ya ADPOLLEX” alisema Bw Daniel Octavian, Meneja Mkuu wa ADPOLLEX Tanzania, huku tukijivunia timu yenye wafanyakazi bora na kazi nzuri ambazo tumeshazifanya mpaka sasa kwa wateja wetu,licha ya kuandaa kazi nzuri zilizoendana na soko la wateja wetu lakini pia tumeonekana kimataifa na kupata nafasi ya kushiriki kwenye baadhi ya forum mbalimbali duniani kwenye sekta ya matangazo. Ushiriki huu utakuwa na manufaa makubwa kwa wateja wetu na kutuwezesha sisi kama ADPOLLEX kupanua wigo wetu wa kufanya kazi kimataifa.
Dhamira yetu ni kuona ushindani wa matangazo ya bidhaa kwa Tanzania unakua na kufikia viwango vya kimataifa.
Bw Daniel aliendeela kusema “Kama kampuni tumefanya kazi hapa Tanzania kwa miaka miwili na makampuni ya ndani na nje ya Tanzania ikiwamo makampuni ya simu, benki, taasisi zisizo za kiserikali,kampuni za samani za ndani, kampuni za sola na nyingine nyingi. Kwa miaka hiyo michache ya kufanya kazi kwa bidii na kutambulika kimataifa,kampuni ya ADPOLLEX sasa inasababu ya kujivunia ujuzi wa kufanya kazi za wazawa huku tukizifanya kwa viwango vya kimataifa. Kama wadau wa matangazo tunaamini ubunifu bora unaleta ushindani katika soko na kuweza kuifikisha bidhaa kwenye viwango vya kimataifa.
GudyTV

Saturday, April 22, 2017

Njia Tano (5) Bora Za Kupata Mtaji Wa Kuanza Au Kukuza Biashara


Moja ya changamoto ambazo watu wengi wanaotutafuta huwa ni wanawezaje kupata mtaji wa kuanza biashara. Hiki kimekuwa kikwazo kwa watu wengi kuingia kwenye biashara. Hata wale ambao tayari wapo kwenye biashara, wamekuwa wakitamani kukuza biashara zao ila wanashindwa kutokana na kukosa fedha za kuingiza kwenye biashara.

Tatizo kubwa ambalo linawazuia wengi kutopata mtaji wa biashara ni kwa sababu inapokuja swala la mtaji wanafikiria sehemu moja tu, ambayo ni mkopo. Na kwa bahati mbaya sana watu wengi wanakuwa hawana sifa zinazowawezesha kupata mkopo wa kibiashara. Kwa kukosa sifa hizo huishia kukaa na kulalamika nataka kuingia kwenye biashara ila mtaji sina.

Kama wewe unapenda biashara, na umepanga kuingia au umeshaingia lakini hujaweza kukuza mtaji wako, hapa tutakupa njia mbalimbali za kupata mkopo kwa ajili ya biashara yako.


  1. Fedha zako binafsi.
Njia nzuri sana kwako kupata mtaji wa biashara ni kwa kuanza kuweka akiba ya fedha zako mwenyewe. Kama umeajiriwa anza utaratibu maalumu wa kuweka kiasi cha fedha pembeni ambacho hutakigusa hata iweje. Baadae unaweza kukitumia kwenye kuanza biashara. Kama hujaajiriwa unaweza kutafuta shughuli yoyote ukafanya na hii ikakuingizia kipato ambacho baadae utaweza kuanzia biashara.


  1. Michango kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki.
Kama unaweza kukaa chini na ndugu zako na ukawashawishi vizuri, watakuwa tayari kukuchangia uanze biashara. Kama watu wanaweza kuchangia harusi na mambo mengine, wanaweza pia kuchangia biashara, ni wewe uweze kuwashawishi vizuri. Ila hapa unahitaji kuwa unaaminika na ndugu hao n apia waoneshe ni jinsi gani wao watanufaika na biashara utakayoanzisha.


  1. Kutafuta mtu au watu wa kushirikiana nao.
Kwa uzoefu wetu, kuna watu wengi ambao wana mitaji ya kibiashara ila hawajui ni biashara gani wafanye au hawana muda wa kusimamia biashara. Na wakianzisha biashara kwa sababu hawana usimamizi mzuri wanapata hasara. Sasa wewe unahitaji kuwajua watu wa aina hii na andaa mpango ambao utawashirikisha na kuonesha ni kwa jinsi gani mkiungana pamoja mnaweza kuwa na biashara nzuri na yenye faida. Hii pia inahitaji uwe unaaminika na yule unayempelekea mpango wako.


  1. Kuanza biashara kwa fedha za mteja.
Hapa unaweza kukusanya fedha kwa wateja kwanza halafu ndio ukawapata huduma au bidhaa wanayohitaji. Kama utaweza kuwa na mpango mzuri wa biashara ambapo mteja anahitaji sana unachotoa, na tayari anakuamini anaweza kukupa sehemu ya gharama na wewe kutumia gharama hiyo kumpatia bidhaa au huduma anayotaka. Hii pia inahitaji uaminifu na wale unaofanya nao biashara.

Hii ndio njia ambayo inafahamika na kila mtu na watu ndio huwa wanaifikiria hii kila wanapofikiria mkopo wa biashara. Kama una sifa za kupata mkopo unaweza kuchukua mkopo na kuutumia kwenye biashara. Ila kuwa makini sana kama unachukua mkopo kwa ajili ya kuanzia biashara, ni hatari sana na unaweza kujiingiza kwenye matatizo zaidi.

Bado unafikiria ni njia gani unazoweza kutumia kupata mkopo wa biashara? Anza na hizo hapo juu na boresha kadiri biashara yako ilivyo na wale wanaokuzunguka walivyo. Hakuna kitu kinachoshindikana kama utaamua kweli kupata mkopo wa biashara.
 

Sunday, March 26, 2017

Siri 5 za kuwa msanii bora na mwenye mafanikio

 

Siku zote mafanikio huwa hayana  kanuni kamili ya kusema kwamba ukiifwatisha  itakutoa bali huwa kuna vitu ambavyo ukivizingatia unaweza fikia mahali pazuri ambako ni nafuu kuliko ulivyozania. Wasanii wengi katika tansia mbali mbali imewachukua mda kutambua nyenzo gani au njia zipi za kupitia ili waweze fikia malengo na jinsi ya kumudu pindi pale wanapofikia hayo malengo. Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo yapaswa kuzingatia ili uweze fikia mafanikio;
 
 
1. Sanaa iwe kiini cha maisha yako

Unapoamka au kabla haujalala inabidi uwe unafikiria kuhusu sanaa, kitu gani kingine ufanye cha sanaa ambacho kikifikia hadhira kiweze kukongoa nyoyo za mashabiki. Muda wako mwingi utumie kufanya sanaa na jinsi ya kuitangazisha ili iweze fikia wengi maana kazi inaweza ikawa nzuri sema hamna njia ya kufikisha kwa walengwa. Kwa maana nyingine sanaa inabidi iwe kazi yako kwa muda wote , ifanye kwa kujiamini na kwa kupenda bila kushurutishwa.

2. Elewa jinsi sanaa inavyokwenda mkabala na biashara

Msanii inabidi aelewe sekta za ujasiriamali katika sanaa ili aweze ingiza kipato kupitia sanaa hiyo. Kunapokuja njia mpya ya kibiashara katika sanaa, msanii hana budi bali kuelewa njia hiyo, ajue atafaidika vipi na haki zake zipi ili ajiunge nayo moja kwa moja au anaweza akayagawa madaraka hayo kwa msimazi au wasimazi wake ili yeye aweze kuendelea na mambo mengine huku wasimazi waweze msaidia kwenye swala hilo. Hii itaokoa muda na hata kumfanya afike mbali zaidi kama akizingatia.

3. Fanya kazi kwa bidii

Unaweza ukawa ni msanii mzuri na unaipenda kazi yako sema ni mvivu katika utekelezaji wa kazi yako. Hii inaweza kukurudisha nyuma kimaendeleo. Msanii unatakiwa uwe unaipenda kazi yako lakini pia uwe na juhudi ya kufanya kazi yako kwa kuwa mafanikio hayaji hivi hivi. Pindi unatakavyojituma pia itawapa mshawasha hata waliopembeni yako kujitoa zaidi kwa kukusaidia kwa kuwa wanaona unamwelekeo. Ukiwa mvivu utabaki pewa sifa tu lakini hausogei kwa namna moja ama nyimgine kimaisha.


4. Kutokata tamaa

Katika sanaa huwa kuna vitu mbali mbali ambavyo lazima msanii akabiliane navyo ili kufikia malengo. Na vitu hivyo huwa vinakulazimu kufanya kazi ya ziada au kufanya kazi kwa bidii maana kuna kupanda na kushuka katika sanaa sasa pindi pale unapokwama haikupasi kukata tama na kughairi kabisa bali inapaswa uichukulie kama changamoto na kisha ifanyie kazi. Huwezi jua, pale unapokatia tamaa kama ungekomaa na kuendelea kidogo mafanikio kumbe yalikua karibu.


5. Kaa na watu wenye mawazo chanya

Usipende kuzungukwa na watu wenye mawazo hasi na wewe sanasana tukija kwenye upande wa sanaa unayoifanya . Utakuta badala watu wakusaidie kimawazo na ushauri, wao cha kwanza ni kukuambia acha sanaa hiyo kwa sababu zisizo na msingi. Jitahidi kukaa na watu wenye mawazo chanya kiasi kwamba anakupa ushari pindi anapoona umeteleza ama jinsi ya kufikia malengo. Wasanii wengi wakongwe wanaweza kuwa msaada kwako wewe msanii chipukizi kwa kuwa wanaufahamu mkubwa na ujuzi ambao unaweza kukusaidia wewe kwa namana moja ama nyingine. Jifunze toka kwao kisha chukua ya kwao changanya na yako na utajikuta unafika mbali bila kutarajia.


Wednesday, August 10, 2016

TANGAZA BIASHARA YAKO NA BAN MARKETZ UPATE WATEJA WENGI ZAIDI


  Ban Marketz inakupa fursa wewe Mfanya Biashara Kuweza kutangaza Biashara yako kwa Bei nafuu na kwa urahisi zaidi.
Tangaza Biashara yako nasi ili uweze kufikia malengo uliyo jiwekea katika Biashara yako, Ban Marketz inauwezo mkubwa wa kutangaza Biashara yoyote ile kama vile Maduka, Bidhaa, Mikutano, Viwanja na Mashamba, Nyumba na Partment. Pia tunapokea matangazo yoyoye isipo kuwa matangazo yasioruhusiwa na serikali yaani kisheria..

Mahitaji yetu ni Picha za Product yako unazo taka kutangaza (zisizidi picha 10 ) na maelezo ya Product yako pamoja na Contact zako na Location Ulipo..

Ban Marketz  ina miliki pages,groups tofauti kwenye social media zote zinazotembelewa kwa sasa inapata PAGE VIEWS (yani Kusomwa mara ) laki 6 mpaka 1,000,000 kwa Siku moja na kwa Mwezi Ban Marketz inapata PAGE VIEWS (Kusomwa mara )Milion 12,500,000 kwa uwezo huu tulionao Ban Marketz itaweza kuitangaza Bishara yako na kuweza kuwafikia watu wengi zaidi ndani na nje ya nchi..
Kwa mawasiliano nasi 0684320325, 0768 320325, 0656704111 Namba zote zinapatikana.

Wednesday, June 8, 2016

Jifunze namna ya kuanzisha biashara yako kwa njia sahihi

Jifunze namna ya kuanzisha biashara Kwenye thread hii nimeona wengi wamepost hoja ya kutaka ushauri wa kuanzisha biashara, na wengine wameenda mbali zaidi kwa kutaja kiwango cha pesa alicho nacho kwamba ni biashara gani itafaa. Lakini inaonyosha dalili kwamba waanzaji wengi wa biashara wanakimbilia kuanzisha biashara kabla ya kupanga mikakati ya utafiti kwa kutumia kigezo cha business plan. Ni dhahiri uanzishwaji wa biashara ambayo itasajiliwa serikalini na kulipia kodi ni tofauti na mfumo wa biashara za kimachinga ambao hununua na kuuza eneo analotaka na sipopata wateja huhamia eneo jingine.

Business Plan ni jambo la kwanza na la msingi katika uanzishwaji wa biashara yako. Mambo ya msingi unayotakiwa kufanya katika business plan yako ni kama ifuatavyo:

  • Aina ya biashara unayokusudia kuanza
  • Wateja walengwa kwa biashara yako wanaoishi maeneo hayo, wanaopita maeneo hayo nk.
  • Eneo la kufanyia biashara yako ukitilia maanani kuchunguza ushindani wa biashara uliopo katika eneo hilo.
  • Fanya utafiti na wafanyabiashra wengine ambao wana uzoefu na biashara hiyo ili kupata mwelekeo wa biashara yako.
  • Fanya utafiti wa source ya kupata bidhaa kutoka makampuni yanayouza na tafiti ni kampuni ipi yenye maslahi kwako.
  • Andaa mfumo wa gharama za uendeshaji wa biashara ikiwa ni pamoja na Mtaji wako,
  • Gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na gharama za uanzaji wa bishara, vitendea kazi, kulipia pango, tax, umeme, usafiri, simu, mishahara, nk. (Kumbuka wewe unalipwa mshahara pia na umeajiriwa na biashara yako).
  • Kisha tathmini faida utakayopata baada ya gharama za uendeshaji na kumbuka biashara inasimama ambayo ina net profit, gross profit tu ni hasara.
Mtaji ulio nao usiuhesabu kama ndio kianzio cha biashara yako, maana kuna gharama za maandalizi ya mahali utakapoweka biashara yako, leseni za biashara pamoja na vitendea kazi vingine. Hivyo vyote uvifanyie mahesabu katika gharama za uanzishwaji wa biashara yako.
Hakikisha theluthi moja ya mtaji wako wa pesa umebaki kwa ajili ya uendeshaji wa biashara yako maana biashara hadi isimame na kuanza kujiendesha yenyewe huchukua wastani wa miezi 6 kama upo eneo lenye wateja wazuri.

Huu ni ushauri wangu binafsi, nategemea kuna wengi hapa wenye ushauri mzuri zaidi watajazia yaliyopungua.