Wednesday, June 8, 2016

Jifunze namna ya kuanzisha biashara yako kwa njia sahihi

Jifunze namna ya kuanzisha biashara Kwenye thread hii nimeona wengi wamepost hoja ya kutaka ushauri wa kuanzisha biashara, na wengine wameenda mbali zaidi kwa kutaja kiwango cha pesa alicho nacho kwamba ni biashara gani itafaa. Lakini inaonyosha dalili kwamba waanzaji wengi wa biashara wanakimbilia kuanzisha biashara kabla ya kupanga mikakati ya utafiti kwa kutumia kigezo cha business plan. Ni dhahiri uanzishwaji wa biashara ambayo itasajiliwa serikalini na kulipia kodi ni tofauti na mfumo wa biashara za kimachinga ambao hununua na kuuza eneo analotaka na sipopata wateja huhamia eneo jingine.

Business Plan ni jambo la kwanza na la msingi katika uanzishwaji wa biashara yako. Mambo ya msingi unayotakiwa kufanya katika business plan yako ni kama ifuatavyo:

  • Aina ya biashara unayokusudia kuanza
  • Wateja walengwa kwa biashara yako wanaoishi maeneo hayo, wanaopita maeneo hayo nk.
  • Eneo la kufanyia biashara yako ukitilia maanani kuchunguza ushindani wa biashara uliopo katika eneo hilo.
  • Fanya utafiti na wafanyabiashra wengine ambao wana uzoefu na biashara hiyo ili kupata mwelekeo wa biashara yako.
  • Fanya utafiti wa source ya kupata bidhaa kutoka makampuni yanayouza na tafiti ni kampuni ipi yenye maslahi kwako.
  • Andaa mfumo wa gharama za uendeshaji wa biashara ikiwa ni pamoja na Mtaji wako,
  • Gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na gharama za uanzaji wa bishara, vitendea kazi, kulipia pango, tax, umeme, usafiri, simu, mishahara, nk. (Kumbuka wewe unalipwa mshahara pia na umeajiriwa na biashara yako).
  • Kisha tathmini faida utakayopata baada ya gharama za uendeshaji na kumbuka biashara inasimama ambayo ina net profit, gross profit tu ni hasara.
Mtaji ulio nao usiuhesabu kama ndio kianzio cha biashara yako, maana kuna gharama za maandalizi ya mahali utakapoweka biashara yako, leseni za biashara pamoja na vitendea kazi vingine. Hivyo vyote uvifanyie mahesabu katika gharama za uanzishwaji wa biashara yako.
Hakikisha theluthi moja ya mtaji wako wa pesa umebaki kwa ajili ya uendeshaji wa biashara yako maana biashara hadi isimame na kuanza kujiendesha yenyewe huchukua wastani wa miezi 6 kama upo eneo lenye wateja wazuri.

Huu ni ushauri wangu binafsi, nategemea kuna wengi hapa wenye ushauri mzuri zaidi watajazia yaliyopungua.

No comments:

Post a Comment