Saturday, April 22, 2017

Njia Tano (5) Bora Za Kupata Mtaji Wa Kuanza Au Kukuza Biashara


Moja ya changamoto ambazo watu wengi wanaotutafuta huwa ni wanawezaje kupata mtaji wa kuanza biashara. Hiki kimekuwa kikwazo kwa watu wengi kuingia kwenye biashara. Hata wale ambao tayari wapo kwenye biashara, wamekuwa wakitamani kukuza biashara zao ila wanashindwa kutokana na kukosa fedha za kuingiza kwenye biashara.

Tatizo kubwa ambalo linawazuia wengi kutopata mtaji wa biashara ni kwa sababu inapokuja swala la mtaji wanafikiria sehemu moja tu, ambayo ni mkopo. Na kwa bahati mbaya sana watu wengi wanakuwa hawana sifa zinazowawezesha kupata mkopo wa kibiashara. Kwa kukosa sifa hizo huishia kukaa na kulalamika nataka kuingia kwenye biashara ila mtaji sina.

Kama wewe unapenda biashara, na umepanga kuingia au umeshaingia lakini hujaweza kukuza mtaji wako, hapa tutakupa njia mbalimbali za kupata mkopo kwa ajili ya biashara yako.


  1. Fedha zako binafsi.
Njia nzuri sana kwako kupata mtaji wa biashara ni kwa kuanza kuweka akiba ya fedha zako mwenyewe. Kama umeajiriwa anza utaratibu maalumu wa kuweka kiasi cha fedha pembeni ambacho hutakigusa hata iweje. Baadae unaweza kukitumia kwenye kuanza biashara. Kama hujaajiriwa unaweza kutafuta shughuli yoyote ukafanya na hii ikakuingizia kipato ambacho baadae utaweza kuanzia biashara.


  1. Michango kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki.
Kama unaweza kukaa chini na ndugu zako na ukawashawishi vizuri, watakuwa tayari kukuchangia uanze biashara. Kama watu wanaweza kuchangia harusi na mambo mengine, wanaweza pia kuchangia biashara, ni wewe uweze kuwashawishi vizuri. Ila hapa unahitaji kuwa unaaminika na ndugu hao n apia waoneshe ni jinsi gani wao watanufaika na biashara utakayoanzisha.


  1. Kutafuta mtu au watu wa kushirikiana nao.
Kwa uzoefu wetu, kuna watu wengi ambao wana mitaji ya kibiashara ila hawajui ni biashara gani wafanye au hawana muda wa kusimamia biashara. Na wakianzisha biashara kwa sababu hawana usimamizi mzuri wanapata hasara. Sasa wewe unahitaji kuwajua watu wa aina hii na andaa mpango ambao utawashirikisha na kuonesha ni kwa jinsi gani mkiungana pamoja mnaweza kuwa na biashara nzuri na yenye faida. Hii pia inahitaji uwe unaaminika na yule unayempelekea mpango wako.


  1. Kuanza biashara kwa fedha za mteja.
Hapa unaweza kukusanya fedha kwa wateja kwanza halafu ndio ukawapata huduma au bidhaa wanayohitaji. Kama utaweza kuwa na mpango mzuri wa biashara ambapo mteja anahitaji sana unachotoa, na tayari anakuamini anaweza kukupa sehemu ya gharama na wewe kutumia gharama hiyo kumpatia bidhaa au huduma anayotaka. Hii pia inahitaji uaminifu na wale unaofanya nao biashara.

Hii ndio njia ambayo inafahamika na kila mtu na watu ndio huwa wanaifikiria hii kila wanapofikiria mkopo wa biashara. Kama una sifa za kupata mkopo unaweza kuchukua mkopo na kuutumia kwenye biashara. Ila kuwa makini sana kama unachukua mkopo kwa ajili ya kuanzia biashara, ni hatari sana na unaweza kujiingiza kwenye matatizo zaidi.

Bado unafikiria ni njia gani unazoweza kutumia kupata mkopo wa biashara? Anza na hizo hapo juu na boresha kadiri biashara yako ilivyo na wale wanaokuzunguka walivyo. Hakuna kitu kinachoshindikana kama utaamua kweli kupata mkopo wa biashara.
 

Sunday, April 2, 2017

MAKOSA MATATU YANAYOZUIA USIPATE WATEJA UNAPOTANGAZA BIASHARA



Kama ungependa kupata wateja na kuongeza mauzo katika kampuni au biashara yako, lazima utambue na kuyaepuka makosa yanayofanya usiuze unapotangaza biashara yako. Wateja na mauzo ndio uhai wa biashara yako.
Makosa nilio ainisha hapa, nina uhakika yanazuia mfanyabiashara asipate wateja pindi anapotangaza. Katika kipindi cha mwanzo mwaka 2015 wakati naanza kufanya biashara na kutafuta Business partners, mauzo yangu na hata kupata Business partners haikuwa kazi rahisi, hadi  nilipogundua haya makosa niliokuwa nikiyafanya na kujifunza jinsi ya kuyaepuka.

 WATU HAWASOMI MATANGAZO YAKO. 

Matangazo ndiyo huanza kuitambulisha biashara kwa wateja wako. Ikiwa utafungua biashara kisha ukatulia au unatangaza lakini watu hawasomi matangazo yako, hakuna atakayejua unatoa huduma au bidhaa au ofa. Kibaya cha jitangaza kizuri cha jiuza, kauli hii ipe kisogo kama biashara ndio inaanza lazima ujue jinsi ya kuitangaza.
Kwa nini watu hawasomi tangazo lako? 

• Headline(kichwa cha tangazo) 

Kama umeweka tangazo  katika Mitandao ya kijamii, barua pepe au umebandika mahali watu wanaliona lakin wanalipita bila kulisoma, hapo tatizo la kwanza lipo kwenye headline (kichwa cha tangazo).
Headline ndio inamfanya msomaji amue ndani ya muda wa sekunde 3 hadi 10 kusimama asome tangazo lako au apitilize. Kwenye Internet wasomaji wanafanya maamuzi haraka sana ndani ya sekunde 3, atakuwa ameamua kusoma makala au tangazo lako au abonyeze kitufe aendelee na safari kulingana na Headline.
Tengeneza vichwa hata zaidi ya vitano vya tangazo lako kisha uchague. Headline ya kwanza kujitokeza kichwani, inaweza isiwe nzuri kuliko utakazo zipata ukiendelea kufikiria.

• Mwanzo wa Tangazo 

Sentensi ya mwanzo baada ya tangazo. Ni muhimu kuwa na mvuto wa kumfanya msomaji atake kuendelea kusoma yaliyomo ndani ya tangazo.
Mfano:
Kama ungependa kupata wateja na mauzo…..
Kama ungependa kupata bidhaa bora na zenyekutatua…..
Sasa unaweza kupata/kupokea/kutumia….
Mifano miwili hapo nimetoa kukupa mwanga, ujifunze jinsi ya kumlazimisha msomaji aendelee kusoma yanayofuata katika tangazo lako.

2. HULENGI WATEJA HUSIKA (BAD TRAGERTING)

Watu watasoma tangazo lako, lakini hutaweza kuwabadili kuwa wateja kama tangazo umeandika vizuri lakini hukufanya utafiti mzuri ni wapi utapata wateja wako.  Unajikuta umepeleka tangazo au bidhaa kwa wasio wahitaji. Ni kana vile umekwenda kutangaza au kuuza Computer kwa ambao hawahitaji na hawaju au kuuza nguruwe msikitini.
Jinsi ya kufanya target ya wateja:

Kabla ya kuanza biashara fanya tafiti kuhusu wateja, unatakiwa kufahamu wateja wako ni akina nani na sifa zao ni zipi. Sifa za kutambua kwa wateja:

Jinsia: Mke/Me
Umri:  18 – 45 (mfano)
Kipato: ********
Elimu: ********

Baada ya kutambua wateja wako, fanya jitihada za kufahamu  wapi utawapata.

Wateja wako wanapatikana sehemu mbalimbali kutegemeana na sifa za wateja wako. Mfano wanaweza patikana:
Magrupu ya ujasiriamali katika mitandao ya kijamii.
Sehemu za michezo
Mashuleni
Katika forum mbalimbali ujasiriamali, michezo, mapenzi, siasa n.k(itategemeana na wewe biashara)
Usipokuwa tambua wateja wako vizuri na kufahamu wapi wanapatikana ndio unajikuta, unapoteza muda kutangaza bidhaa au huduma kwa watu ambao hawatumii biashara yako.
Watu wananunua au kulipia vitu ambavyo wanafikri vitatua matatizo walio nayo. Wananunua vitu wanavyohitaji wanaacha ambavyo hawahitaji. Hivyo ili uuze lazima ufanye target ya wateja, ukitaka kila mtu umuuzie utatumia muda na pesa yako lakini matokeo yanakuwa hafifu.

Hatua ya tatu ni kuweka mikakati ya kufika mahali wateja wako walipo.

Katika hatua hii ndio unaandaa matangazo kwa kuzingatia sifa za wateja wako kisha unapeleka tangazo mahali walipo.

3.  HUTOI OFA KWA WATEJA

Ofa inamfanya mteja ambaye hajawahi kuitumia bidhaa au huduma yako kupata nafasi ya kuijaribu huduma au biashara yako. Mteja anakuwa na mashaka na ubora wa bidhaa yako na wewe mwenyewe muuzaji.
Nini cha kufanya kumwondoa hofu mteja?

Kama mteja ana hofu na wewe, jitihadi kuwa unajifunza mbinu, maswali na jinsi ya kumsaidia mteja kufikia maamuzi ya kufanya manunuzi.
Unapotangaza biashara yako kumbuka kuweka ofa, chagua ofa ambayo haikuathiri, ofa zipo nyingi sio lazima utoe bidhaa zako bure 100%, unaweza:
Kuanza kutoa thamani ya huduma yako, wateja wako wakikuamini basi wanakujoin.
Toa punguzo katika kipindi maalumu, baada ya muda husika wa ofa, rudisha bei kama ilivyokuwa.
Ukitoa ofa ya punguzo toa tangazo. Kumbuka kuweka muda wa mwisho wa ofa. Muda wa mwisho unapokaribia mteja akiona tangazo huwa anahamasika kufanya maamuzi ikiwa tangazo linamhusu.


4. BIDHAA/HUDUMA YAKO HAIKIDHI HITAJI LA MTEJA

Je, mteja wako anapata alichotarajia kupata wakati akinunua huduma yako?? Kama umelenga vema wateja husika, lakini bidhaa hazina ubora au hazitatui hutaji husika la mteja, kuna uwezekano wa kupoteza wateja. Mteja hataweza kurudi kununua bidhaa yako kama alinunua akakutana na hali ambayo haikumridhisha.
Fanya jitihada tangu unapoanza biashara, chagua biashara ambayo itagusa wengi, kama ni huduma toa huduma anbayo itagusa wengi.
Kwa makala nyingine kuhusu masoko na mbinu za kupata wateja kupitia mitandao ya kijamii, tembelea page yangu: Shori MN(page)  au blog: shori success life