Siku zote mafanikio huwa hayana kanuni kamili ya kusema kwamba ukiifwatisha itakutoa bali huwa kuna vitu ambavyo ukivizingatia unaweza fikia mahali pazuri ambako ni nafuu kuliko ulivyozania. Wasanii wengi katika tansia mbali mbali imewachukua mda kutambua nyenzo gani au njia zipi za kupitia ili waweze fikia malengo na jinsi ya kumudu pindi pale wanapofikia hayo malengo. Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo yapaswa kuzingatia ili uweze fikia mafanikio;
1. Sanaa iwe kiini cha maisha yako
Unapoamka
au kabla haujalala inabidi uwe unafikiria kuhusu sanaa, kitu gani
kingine ufanye cha sanaa ambacho kikifikia hadhira kiweze kukongoa nyoyo
za mashabiki. Muda wako mwingi utumie kufanya sanaa na jinsi ya
kuitangazisha ili iweze fikia wengi maana kazi inaweza ikawa nzuri sema
hamna njia ya kufikisha kwa walengwa. Kwa maana nyingine sanaa inabidi
iwe kazi yako kwa muda wote , ifanye kwa kujiamini na kwa kupenda bila
kushurutishwa.
2. Elewa jinsi sanaa inavyokwenda mkabala na biashara
Msanii
inabidi aelewe sekta za ujasiriamali katika sanaa ili aweze ingiza
kipato kupitia sanaa hiyo. Kunapokuja njia mpya ya kibiashara katika
sanaa, msanii hana budi bali kuelewa njia hiyo, ajue atafaidika vipi na
haki zake zipi ili ajiunge nayo moja kwa moja au anaweza akayagawa
madaraka hayo kwa msimazi au wasimazi wake ili yeye aweze kuendelea na
mambo mengine huku wasimazi waweze msaidia kwenye swala hilo. Hii
itaokoa muda na hata kumfanya afike mbali zaidi kama akizingatia.
3. Fanya kazi kwa bidii
Unaweza
ukawa ni msanii mzuri na unaipenda kazi yako sema ni mvivu katika
utekelezaji wa kazi yako. Hii inaweza kukurudisha nyuma kimaendeleo.
Msanii unatakiwa uwe unaipenda kazi yako lakini pia uwe na juhudi ya
kufanya kazi yako kwa kuwa mafanikio hayaji hivi hivi. Pindi
unatakavyojituma pia itawapa mshawasha hata waliopembeni yako kujitoa
zaidi kwa kukusaidia kwa kuwa wanaona unamwelekeo. Ukiwa mvivu utabaki
pewa sifa tu lakini hausogei kwa namna moja ama nyimgine kimaisha.
4. Kutokata tamaa
Katika
sanaa huwa kuna vitu mbali mbali ambavyo lazima msanii akabiliane navyo
ili kufikia malengo. Na vitu hivyo huwa vinakulazimu kufanya kazi ya
ziada au kufanya kazi kwa bidii maana kuna kupanda na kushuka katika
sanaa sasa pindi pale unapokwama haikupasi kukata tama na kughairi
kabisa bali inapaswa uichukulie kama changamoto na kisha ifanyie kazi.
Huwezi jua, pale unapokatia tamaa kama ungekomaa na kuendelea kidogo
mafanikio kumbe yalikua karibu.
5. Kaa na watu wenye mawazo chanya
Usipende
kuzungukwa na watu wenye mawazo hasi na wewe sanasana tukija kwenye
upande wa sanaa unayoifanya . Utakuta badala watu wakusaidie kimawazo na
ushauri, wao cha kwanza ni kukuambia acha sanaa hiyo kwa sababu zisizo
na msingi. Jitahidi kukaa na watu wenye mawazo chanya kiasi kwamba
anakupa ushari pindi anapoona umeteleza ama jinsi ya kufikia malengo.
Wasanii wengi wakongwe wanaweza kuwa msaada kwako wewe msanii chipukizi
kwa kuwa wanaufahamu mkubwa na ujuzi ambao unaweza kukusaidia wewe kwa
namana moja ama nyingine. Jifunze toka kwao kisha chukua ya kwao
changanya na yako na utajikuta unafika mbali bila kutarajia.
No comments:
Post a Comment